|
Makomandoo wa Kikosi Maalumu cha Majini cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) |
|
Thursday, 02 September 2010 12:47 |
|

Makomandoo wa Kikosi Maalumu cha Majini cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakifanya onesho la uokoaji wa mateka kwenye 'Kisiwa' jana ikiwa ni sehemu ya ufungaji wa maadhimisho ya miaka 46 ya jeshi hilo. (Picha na Charles Lucas) |
|
|
Thursday, 02 September 2010 12:39 |
|
Na Waandishi Wetu, jijini/Morogoro
UMATI wa ndugu uliojaa simanzi ulifurika jana katika makaburi ya Kola, mjini Morogoro baada ya moto kuzuka ghafla na kuteketeza zaidi ya makaburi 100.
Baadhi ya ndugu walifika eneo hilo walijikuta wakiangua vilio baada ya kushuhudia moto huo ukiendelea kushika kasi katika makaburi hayo ya Wakristo huku ukiteketeza misalaba yote na uharibifu mwingine katika makaburi hayo.
|
|
Makamba amcharukia Shibuda |
|
Thursday, 02 September 2010 12:30 |
|
Na Dunstan Bahai,Jijini
KATIKA hali inayoonesha joto la kampeni za uchaguzi linazidi kupanda, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, amemjia juu mgombea Ubunge wa Jimbo la Maswa Magharibi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Shibuda, na kumfananisha na ‘mwenda wazimu’.
|
|
|
Maisha ya Watanzania mashakani |
|
Thursday, 02 September 2010 12:35 |
|
Na Christina Gauluhanga, jijini
WANANCHI wameingiwa na hofu kuhusu afya zao baada ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kutangaza rasmi kuruhusu matumizi ya dawa ya Meltakelfin kutoka Italia ambayo ilipigwa marufuku kwa madai kuwa hazikukidhi viwango vya ubora uliotakiwa.
|
|
CHADEMA yazidi kumkalia kooni JK |
|
Tuesday, 31 August 2010 11:23 |
|
Na Grace Ndossa, jijini
MSAJILI wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa, amesema amepokea pingamizi la malalamiko ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) dhidi ya mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo asubuhi, Tendwa amesema uamuzi wa pingamizi hilo juu ya Sheria za Gharama za Uchaguzi utatolewa baada ya siku tano ambapo ataita pande zote mbili ili ziweze kutoa maelezo ya kina.
Ameongeza kuwa baada ya kusikiliza pande zote atawasilisha nakala kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi pamoja na makatibu wakuu wa vyama vyote viwili.
Amesema sheria ya gharama za uchaguzi ni tofauti na Ilani ya Chama, hivyo baada ya uamuzi huo ambaye hataridhika ana haki ya kwenda kwenye chombo cha sheria kwa ajili ya kutafuta haki zaidi.
CHADEMA iliazimia kumwekea pingamizi mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Rais Jakaya Kikwete, kwa madai kuwa amekiuka sheria ya gharama za uchaguzi kwa kutangaza nyongeza ya mishahara kwenye kampeni na hivyo azuiwe kugombea urais.
|
|
|
|
|
<< Start < Prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 Next > End >>
|
|
Page 1 of 47 |