Home
Dar Leo
Mwanafunzi afa maji akienda kusalimia
Monday, 30 August 2010 13:02

Na Christina Gauluhanga, Polisi

OMARY Mohamed (9), mwanafunzi wa darasa la tatu kutoka Shule ya Msingi Tandika Azimio, mkazi wa Tandika, amekufa baada ya kuzama maji wakati akiogolea mto Kizinga, Kivule wilaya ya Ilala.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Missime, amesema tukio hilo limetokea jana saa 7 mchana Mto Mzinga.

Imedaiwa kuwa mwanafunzi huyo na mama yake, Amina Omary (30), mkazi wa Tandika, walikwenda Kivule kusalimia ndugu zao ambapo mtoto huyo alitoka na kwenda kuogelea na wenzake.

 
Mgombea aahidi kuineemesha Ukonga
Monday, 30 August 2010 13:01

Stella Aron na Christina Gauluhanga, Ukonga

MGOMBEA ubunge Jimbo la Ukonga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eugen Mwaiposa, amewaasa wananchi wa jimbo hilo kukipigia kura chama hicho ili kuweza kubadilisha sura ya jimbo hilo na kuleta maendeleo ya haraka.

Akizungumza na gazeti hili, mgombea huyo amejigamba kuwa endapo atachaguliwa kuingia atahakikisha kuwa wananchi wa jimbo hilo wanapata maji ya bomba.

 
Mchinga kizimbani akidaiwa kuiba magari
Monday, 30 August 2010 12:58

Na Halima Kilagu, Temeke

MSHITAKIWA Yahya Mchinga (26), mkazi wa Kurasini, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Temake kujibu mashitaka ya wizi wa gari.

Mshitakiwa amesomewa mashitaka na Mwendesha Mashitaka Issaya Mwanga mbele ya Hakimu Rose Kagwa.

Imedaiwa mahakamani hapo kuwa Agosti 2, mwaka huu, saa 6 usiku, mshitakiwa aliiba gari mbili aina ya Isuzu zenye thamani ya sh. 50,000,000, mali ya Adolf Emmanuel.

 
Wanafunzi waanguka mashetani
Monday, 30 August 2010 13:00

Na Khadija Idd, Tabata

VILIO na simanzi vimetawala leo katika Shule ya Msingi Tumani ambako zaidi ya wanafunzi 26 wameanguka ghafla na kuanza kupiga mayowe wakidai wanawaona watu walio uchi wa mnyama.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu tukio hilo limetokea leo saa 2 asubuhi ambapo wazazi na walezi walilazimika kutinga katika shule hiyo kwa ajili ya kuokoa maisha ya watoto wao.

Hali hiyo imezua tafrani kati ya wazazi na walimu hao ambapo kwa msaada wa haraka walikuwa wakiwachukua watoto wanaodondoka kisha kuwakimbiza kwenye kanisa la Assembles Of God lililopo jirani kwa ajili ya kuombewa.

 
Kimanga waomba barabara zifanyie ukarabati
Monday, 30 August 2010 12:51

Na Shaaban Mkumbwa, Tabata

WAKAZI wa Kimanga Darajani wameiomba Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Serikali ya Mtaa kukarabati barabara ambazo zimekuwa kero kwa kipindi kirefu kutokana na kushindwa kupitika.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wakazi hao wamedai kuwa barabara hizo ziliharibiwa na mvua na kusababisha kuwapo kwa madimbwi yanayosababisha kero wa madereva na kusababisha kuwepo kwa kero ya usafiri.

Wamedai kuwa kutokana na kuwepo kwa mashimo hayo hivi sasa katika barabara itokayo kituo cha Savana kuelekea Tabata AMI haipitiki kutokana na kuwapo kwa mashimo makubwa.

 
<< Start < Prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 Next > End >>

Page 3 of 47

Swali la Leo

Website is used for?
 

Walio Kwenye Mtandao

We have 12 guests online
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday521
mod_vvisit_counterYesterday768
mod_vvisit_counterThis week1695
mod_vvisit_counterLast week5276
mod_vvisit_counterThis month4732
mod_vvisit_counterLast month22527
mod_vvisit_counterAll days53352

We have: 11 guests, 1 bots online
Your IP: 38.107.191.105
 , 
Today: Sep 07, 2010