|
Friday, 27 August 2010 11:53 |
|
*Mwanamke abambwa wodi ya wazazi *Akutwa na nyama pamoja na moyo wa ng'ombe *Pia ametota rangi nyekundu
Christina Gauluhanga na Stella Aron, jijini
VITIMBWI na hekaheka jana zilitawala katika wodi ya wazazi baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Habiba Shabaan (19), mkazi wa Mbagala kwa Mangaya, kunaswa akiwa na kipande cha nyama ya ng'ombe na moyo wa mnyama huyo.
Shuhuda wetu amedai kuwa, tukio hilo limetokea jana saa 4 asubuhi, hospitalini hapo.
Imedaiwa kuwa mwanamke huyo alienda hospitalini hapo akiwa hoi haitambui akidai kuwa, ameshikwa na uchungu hivyo muuguzi wa zamu Catheline Paulo (28), alimpokea na kumpeleka wodini hapo.
|
|
|
Jambazi lauawa na wananchi |
|
Friday, 27 August 2010 11:52 |
|
*Ni baada ya kuiba mil.12/- za Saccos
Na Waandishi Wetu, Tanga
KUNDI la majambazi wakiwa na silaha limevamia ofisi ya Ushirika wa Kuweka na Kukopa (Saccos) mkoani Tanga na kuiba sh. milioni 12.
Hata hivyo, wananchi wamefanikiwa kuliua jambazi mojawapo katika mapigano makali ya kurushiana risasi.
Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, tukio hilo limetokea jana mchana katika ofisi za Saccos hiyo zilizopo Tanga Mjini.
|
|
Polisi yamng'ang'ania aliyeiba mtoto |
|
Friday, 27 August 2010 11:48 |
*Inadaiwa mume alikuwa akitaka wa kiume *Yeye amezaa wa kike
Na Waandishi Wetu, jijini
POLISI inamshikilia mwanamke mmoja (jina tunalo), mkazi wa Tabata, aliyeiba mtoto mchanga katika Hospitali ya Temeke baada ya kuwarubuni wazazi wa mtoto huyo hospitalini hapo.
Tukio hilo lilitokea Aprili 20, mwaka huu, baada ya mwanamke huyo kujifanya ni msamaria mwema na kisha kutoroka na kichanga hicho, Ramadhani Rashid, ambacho sasa kina umri wa miezi minane katika mazingira ya kutatanisha.
|
|
|
Boti iliyosheheni mafuta yawaka moto |
|
Friday, 27 August 2010 11:50 |
|
*Abiria wanusurika kufa *Mali zote zateketea
Na Waandishi Wetu, Mwanza
ABIRIA waliokuwa wakisafiri katika boti iliyokuwa imesheheni mafuta na bidhaa nyingine wamenusurika kufa baada ya boti hiyo kuteketea kwa moto katika Ziwa Victoria, mkoani Mwanza.
Tukio hilo limetokea leo alfajiri Kilumba ambapo moto huo uliteketeza mali zote na inadaiwa kuwa chanzo chake ni hitilafu iliyoanzia kwenye injini.
Shuhuda wetu amedai kuwa boti hiyo, mali ya Omary Ungarobo, ilikuwa inaenda kisiwa cha Ukerewe kupeleka bidhaa hizo ambazo ziliteketea zote.
|
|
Bodaboda mwiba kwa daladala |
|
Friday, 27 August 2010 11:44 |
|
Na Humphrey Shao, Karikaoo
KUONGEZEKA kwa huduma ya usafiri wa bodaboda kumeathiri kipato cha wenye daladaka kutokana na baadhi ya abiria kutumia usafiri huo.
Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili, mmoja wa madereva hao, Seif Mbange, alisema bodaboda hizo ambazo zimekuwa zikiegeshwa katikati ya jiji majira ya jioni kumewaathiri kwa kuwa abiria wengi huzitumia kwa wakati huo kwa kuepuka usumbufu wa foleni.
Alisema idadi ya abiria imekuwa ikipungua siku ahadi siku hasa kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu ambapo abiria wengi ukimbilia bodaboda hizo na kuacha daladala kiasi kinacho athiri kipato chao.
|
|
|
|
|
<< Start < Prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 Next > End >>
|
|
Page 5 of 47 |