Home
Dar Leo
Liverpool, Man City zapeta Europa
Friday, 27 August 2010 11:37

LONDON, England
TIMU za soka za England, Liverpool na Manchester City, zimefuzu kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Europa baada kushinda mechi zao usiku wa kuamkia leo.

Timu hizo zinaungana na vigogo wengine wa Italia Juventus, Napoli na Palermo.

Pia, timu za Ujerumani Borussia Dortmund, Bayer Leverkusen na Stuttgart zimesonga mbele, lakini Celtic, Galatasaray, Fenerbahce, Feyenoord na Aston Villa zimeaga michuano hiyo.

Liverpool iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Trabzonspor ya  Uturuki na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-1, wakati Man City iliibamiza Timisoara mabao 2-0 na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-0.

 
Hapa sheria yasemaje?
Thursday, 26 August 2010 11:08

Daladala namba T159 BFU likilazimika kuingia njia ya watembea kwa miguu kukwepa makalavati yaliyovunjika kwenye eneo la Shule ya Msingi Uhuru Wasichana jana. Kituo hicho kimeachwa muda mrefu bila kufanyiwa ukarabati, jambo linalosababisha usumbufu kwa daladala zinazoegeshwa eneo hilo. (Picha na Zuberi Mussa)

 
Sangoma auawa
Thursday, 26 August 2010 10:58

Na Waandishi Wetu, Mwanza

WANANCHI wenye hasira kali Mkoani Mwanza wamempiga kisha kumchoma moto mganga wa kienyeji, Fikiri Philipian (36), ambaye anadaiwa kumuiba mtoto Magreth Seif (8).

Tukio hilo limetokea jana saa 8:40 mchana katika Tarafa ya Ukara, Ukerewe mkoani Mwanza, baada ya mganga huyo kwenda kumtibia mtoto huyo nyumbani kwa wazazi wake katika kijji hicho.

Imedaiwa kuwa baada ya kumtibia, mganga huyo alimchukua mtoto huyo kutoka kwa wazazi wake ili aende naye nyumbani kwake kwa ajili ya matibabu zaidi.

 
Lipumba 'anusurika' kuanguka jukwaani
Thursday, 26 August 2010 11:05

*Alikuwa akizindua kampeni
*Awaacha hoi wanachama wake
*Vicheko vyatawala

Christina Gauluhanga na Stella Aron, Buguruni

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Ibrahim Lipumba, jana aliuacha hoi umati wa wanachama wake waliokuwa wamefurika katika mkutano wa kampeni wa chama hicho baada ya Mgombea Udiwani wa Vingunguti, Ally Omary, kutikisa jukwaa lake na kuliyumbisha.

Lipumba alipigwa na butwaa na kuuchekesha umati wa watu akidai kuwa alidhani naye zamu yake ya kuanguka imefika, hali ambayo iliwafanya wananchi waliokuwa wamefurika katika viwanja vya Buguruni Kisiwani kuangua vicheko.

 
Maiti yagombea Dar
Thursday, 26 August 2010 10:56

*Yabaki sita
*Wana ndugu nusra watwangane makonde

Na Waandishi Wetu, Kinondoni

SHAURI la madai dhidi ya maiti ya marehemu Onesmo Gasto Kazahura, mkazi wa Mbezi Louis, imefunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni na mke wake, Joyce Owenya, na ndugu zake ambao wanaishtaki Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuzuia maiti ya ndugu yao.

Imedaiwa kuwa marehemu huyo, kabla ya kifo chake, aliandika wosia akiomba kuwa endapo ikatokeo bahati mbaya akafa anaomba maiti yake izikwe hapahapa Dar es Salaam huku familia nyingine ikitaka ikazikwe Bukoba.

 
<< Start < Prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 Next > End >>

Page 6 of 47

Swali la Leo

Website is used for?
 

Walio Kwenye Mtandao

We have 16 guests online
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday462
mod_vvisit_counterYesterday768
mod_vvisit_counterThis week1636
mod_vvisit_counterLast week5276
mod_vvisit_counterThis month4673
mod_vvisit_counterLast month22527
mod_vvisit_counterAll days53293

We have: 14 guests, 2 bots online
Your IP: 38.107.191.106
 , 
Today: Sep 07, 2010