|
TBL yajitumbukiza Bongo Star Search |
|
Thursday, 26 August 2010 10:49 |
|
Na Victor Mkumbo, Posta
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), imeingia mkataba wa miaka mitatu wa kudhamini mashindano ya muziki ya Bongo Star Search yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Akizungumza na gazeti hili, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, alisema wameamua kuingia mkataba huo kwa miaka mitatu baada ya kuona mafanikio yanayopatikana kila mwaka kupitia mashindano hayo.
Amesema mashindano ya Bongo Star Search, hufanyika kila mwaka kwa kushirikisha wasanii kutoka mikoa mbalimbali kwa kuwainua kimuziki na kuwapatia ajira.
|
|
|
Wednesday, 25 August 2010 11:05 |
|
 Baadhi ya wafanyabiashara na madalali wa Mihogo kwenye Soko la Buguruni wakijadiliana kuhusu biashara hiyo wakiwa juu ya magari yenye shehena ya bidhaa hiyo jana. (Picha na Charles Lucas)
|
|
Wednesday, 25 August 2010 11:02 |
|
*Wadai aliyeteuliwa si kijana *Adaiwa kukumbatiwa na vibosile
Na Mwandishi Wetu, jijini
BAADHI ya wajumbe wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoani Arusha, wanapinga uteuzi wa Catherine Magige kuuwakilisha umoja huo bungeni kwa madai kuwa hastahili kutokana na umri wake kuwa zaidi ya miaka 30.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki, wajumbe hao ambao hawakupenda kaundikwa majina yao gazetini, walisema uteuzi wa Catherine unawashangaza kwa kuwa umri wa mjumbe huyo wa UVCCM umevuka ule unaotakiwa na kwamba anatumia jina ambalo si lake.
“Kwa kweli tunashangazwa na Catherine kupewa nafasi ya kutuwakilisha bungeni wakati kuna mambo mengi ambayo yanambana. Tayari umri wake unamuengua katika nafasi hiyo, hivyo tuna wasiwasi na uteuzi wake,” alisema mmoja wa wajumbe hao.
Mjumbe huyo alisema hata watu waliosoma naye katika Shule ya Sekondari ya Ngarenaro jijini Arusha, ambao wanamjua vizuri tangu alipoacha shule akiwa kidato cha pili, nao wameshangazwa na uteuzi wa Catherine.
|
|
|
Tendwa avishukia vyama vya siasa |
|
Wednesday, 25 August 2010 11:03 |
|
*Adai wengine ni wababaishaji *Asema wanajidhalilisha *Apendekeza Katiba ibadilishwe
Stella Aron na Christina Gauluhanga, jijini
MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, amevishukia baadhi ya vyama vya siasa vinavyozusha kuwa wamewekewa mizengwe katika operesheni ya uchukuaji na urejeshaji fomu.
Akizungumza leo asubuhi katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC 1), Tendwa amesema kuwa malalamiko ya wanasiasa hao hayana ukweli wowote kwa kuwa fomu zilianza kutolewa mapema kwenye ofisi za Wakurugenzi wao hivyo walipaswa kwenda kuchukua huko badala ya kulalamika.
Pia amesema haikuwa sahihi kwa wanasiasa hao kulalamikia fomu kwa kuwa uzembe umefanyika kwenye ofisi zao.
|
|
Wanafunzi VS Waendesha pikipiki |
|
Wednesday, 25 August 2010 11:01 |
|
*Watwangana makonde mchana kweupe
*FFU watanda na kutembeza mkong'oto
*Chanzo ni Black Mamba
Na Godfrey Ismaely, jijini
HALI isiyokuwa ya kawaida ilijitokeza katika Shule ya Sekondari Temboni baada ya kuzuka mapambano kati ya waendesha pikipiki na wanafunzi kwa kile kilichodaiwa kuwa dereva mwenzao wa pikipiki katekwa na wanafunzi hao.
Tukio hilo lilitokea jana saa 6 mchana baada ya madereva wa pikipiki kukdaiwa kwenda kuvamia shule hiyo na kuanza kuwashambulia wanafunzi kwa mawe wakiwa madarasani.
|
|
|
|
|
<< Start < Prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 Next > End >>
|
|
Page 8 of 47 |