Home
Dar Leo
Yanga: Tutazidisha makali
Wednesday, 25 August 2010 10:56

Na Winfrida Ngonyani, jijini

UONGOZI wa klabu ya Yanga umetamba kwamba, utaendeleza makali yao katika mechi zote za Ligi Kuu Bara iliyaonza wiki iliyopita.

Yanga, Jumamosi iliichapa Polisi Dodoma bao 1-0, itashuka tena uwanjani Septemba 11, kuumana na AFC ya mjini Arusha ambayo ilijeruhiwa na Azam FC kwa mabao 2-0.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa klabu hiyo,  Louis Sendeu, alisema wakati wachezaji wao saba wakiwa katika kikosi cha timu ya Taifa 'Taifa Stars', waliobaki wataendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Kaunda, Jangwani.

 
Chuji fiti Stars
Wednesday, 25 August 2010 10:52

Na Humphrey Shao, Karume

KOCHA Mkuu wa Taifa 'Taifa Stars' Jan Poulsen amethibitisha kuwa,  kiungo wa timu hiyo Athumani iddi 'Chuji' yuko fiti na ameanza mazoezi katika kikosi chake jana jioni kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Poulsen alisema Chuji ambaye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa malaria na kuwekewa maji, amepata nafuu na tayari amejiunga na wenzake kambini.

Alisema kiungo huyo alifanyiwa vipimo vya damu na daktari wa timu hiyo na kubainika kuwa, amepona na  kujiunga na wenzake.

"Amepona na tayari ameanza mazoezi, namtegemea sana uwanjani," alisema Poulsen.


 

 
CUF yavuna wanachama CCM, CHADEMA
Tuesday, 24 August 2010 12:29

Na Waandishi Wetu, jijini

BAADA ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA) kuwabwaga baadhi ya wagombea katika nafasi za ubunge na udiwani, wagombea wa vyama hivyo wameanza safari ya kuhamia Chama cha Wananchi (CUF), ili kuomba ridhaa ya kugombea katika nafasi mbalimbali.

Afisa Uhusiano wa CUF, Ashura Mustapha, ameliambia gazeti hili leo asubuhi kuwa wanachama hao wameamua kuhamia CUF baada ya kuona wanawekewa mizengwe katika vyama vyao wakati wana sifa zinazostahili kugombea nafasi mbalimbali.

 
NGUMI NDANI YA DALADALA!
Tuesday, 24 August 2010 12:31

Abiria hawa (kinamama) ambao majina yao hayakufahamika wakipigana ndani ya daladala eneo la Kariakoo, Dar es Salaam jana. Haikufahamika mara moja chanzo cha ugomvi wa kinamama hao uliomfanya mmja wao kuchaniwa nguo. (Picha na Prona Mumwi)

 
Alibino aviziwa kuawa
Tuesday, 24 August 2010 12:26

Na Waandishi Wetu, Pwani

MLEMAVU wa ngozi, Thomas Diwani (40), mkazi wa Kibaha kwa Mathias, amenusurika kuuawa na wafanyabiashara baada ya kumvamia nyumbani kwake usiku wa manane kwa ajili ya kumtega ili wapate viungo vyake.

Kwa mujibu wa mlemavu huyo, wafanyabiashara hao walivamia nyumbani kwake majira ya kati ya saa 8 na saa 9 usiku kwa nia ya kumuomba atoke nje ili awasaidie sh. 20,000 kwa ajili ya nauli.

Amedai kuwa akiwa ndani kwake alianza kubishana na wafanyabiashara hao ambao walikuwa wakimlazimisha atoke nje lakini naye aliwaahidi kuwa hawezi kutoka kwa muda huo na kama wataweza wamsubiri nje hadi asubuhi.

 
<< Start < Prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 Next > End >>

Page 9 of 47

Swali la Leo

Website is used for?
 

Walio Kwenye Mtandao

We have 10 guests online
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday481
mod_vvisit_counterYesterday768
mod_vvisit_counterThis week1655
mod_vvisit_counterLast week5276
mod_vvisit_counterThis month4692
mod_vvisit_counterLast month22527
mod_vvisit_counterAll days53312

We have: 4 guests, 6 bots online
Your IP: 38.107.191.106
 , 
Today: Sep 07, 2010