Home
Dar Leo
Nauli zawakwaza madereva
Tuesday, 24 August 2010 12:21

Na Nuru Mwakisyala,Tandika

MADEREVA wa daladala zinazofanya safari zake kati ya Tandika - Ubungo na Tandika - Mwenge wamewaomba abiria kuheshimu viwango vya nauli vilivyowekwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA), ili kuepuka malumbano ya mara kwa mara.

Wakizungumza na gazeti hili madereva hao wamesema kuwa, wanakabiliwa na kero hiyo kutoka kwa abiria wengi wanaotumia usafiri huo kwani kila mmoja anapanga kiwango chake cha nauli jambo ambalo limekuwa likizua ugomvi kila kukicha ndani ya daladala.

 
Rage ambeba Ochan
Tuesday, 24 August 2010 12:15

Na Zahoro Mlanzi, Msimbazi

MWENYEKITI wa klabu ya Simba, Ismail Rage amesema kushindwa kung'ara kwa mshambuliaji wao mpya Patrick Ochan, si kwamba hana uwezo bali bado hajazoea mazingira ya soka la Tanzania.

Ochan alisajiliwa na Simba akitokea St. George ya Ethiopia msimu huu pamoja na wachezaji wengine Amir Maftah aliyekuwa Yanga, Shija Mkina kutoka Kagera Sugar, Salum Aziz 'Gila' akitokea Toto African, Rashid Gumbo na Mbwana Samatta wakitokea African Lyon.

 
TUCTA lakebehi kauli ya JK
Monday, 23 August 2010 11:48

Na Job Ndomba,Jijini

SHIRIKISHO la Vyama Vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) limesema kwamba kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwa ni matusi kudai kuwa hajali wafanyakazi shirikisho hilo limeibuka na kudai kuwa hizo ni kampeni.

Akizugumza na gazeti hili leo asubuhi Katibu wa shirikisho hilo Nicholaus Mgaya amesema kuwa hivi sasa hawatatoa maoni yoyote zaidi ya kumwacha aendelee na kampeni zake.

 
Majiko:
Monday, 23 August 2010 11:50

Mwendesha mkokoteni akipita Mtaa wa Makamba akiwa amejaza majiko akipeleka sokoni kutafuta wateja kama alivyokutwa, Dar es Salaam jana. (Picha na Zuberi Mussa)

 
Makahaba washushiwa dongo
Monday, 23 August 2010 11:46

Bryceson Mathias, Dodoma
 
MHUBIRI wa Neno la Mungu Mwinjilisti Lear Silamu Sibaya amewakemea watu wanaojishughulisha na ukahaba na wale wale wanaovaa nguo fupi zenye mipasuo na milegezo waache mara moja kwa sababu wanatuchafulia nchi yetu yenye heshima.
 
Akizungumza na gazeti hili jana kwenye mkutano wa Injili uliofanyika katika viwanja vya Kanisa la Pentekoste Hollness Assemblies (PHA), mkoani Dodoma, Sibaya alisema kuwa, uvaaji wa aina hiyo unavunja maadili na haumpendezi pia Mungu.

 
<< Start < Prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 Next > End >>

Page 10 of 47

Swali la Leo

Website is used for?
 

Walio Kwenye Mtandao

We have 12 guests online
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday492
mod_vvisit_counterYesterday768
mod_vvisit_counterThis week1666
mod_vvisit_counterLast week5276
mod_vvisit_counterThis month4703
mod_vvisit_counterLast month22527
mod_vvisit_counterAll days53323

We have: 9 guests, 3 bots online
Your IP: 38.107.191.108
 , 
Today: Sep 07, 2010