|
Barabara za mitaa ya Chang'ombe ni 'mahandaki' |
|
Monday, 23 August 2010 11:27 |
|
Na Salim Nyomolelo,Chang'ombe
WAKAZI wa Mtaa wa Bora Kata ya Chang'ombe, wamelalamikia ubovu wa barabara za mtaa huo na kuiomba Manispaa ya Temeke kuzikarabati kwa kushirikiana na wananchi.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, wamesema miaka saba iliyopita barabara zilikuwa zimejengwa kwa kiwango cha lami, lakini kwa sasa zimeharibika vibaya na hazina ukarabati wowote.
|
|
|
Thursday, 19 August 2010 11:16 |
|

Dereva wa Lori la Unga wa Ngano wa Azam, namba T 583 ACY, amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akiendesha kuacha njia na kugonga mti mkubwa, katikati ya Barabara ya Nyerere, eneo la Mtava, Dar es Salaam leo asubuhi. (Picha na Nyakasagani Masenza) |
|
Kiongozi CUF adondosha machozi hadharani |
|
Thursday, 19 August 2010 11:13 |
|
Rehema Maigala na Rachel Balama.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Haji Duni, ameshindwa kuendelea na mkutano baada ya kuangua kilio jukwaani na kudai kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeshindwa kuweka matunda mazuri kwa wananchi wake katika kipindi chote cha utawala wake.
Duni alitokwa machozi hayo baada ya kumwona mama mmoja aliyevamia mkutano huo uliofanyika katika kiwanja cha Bakheresa jijini, akiwa amelewa pombe na huku amebeba mtoto mgongoni huku mtoto huyo akilia njaa.
|
|
|
Wagombea urais wafunika jiji |
|
Thursday, 19 August 2010 11:14 |
|
*Shughuli zasimama kwa muda
*Wapambe nao wafanya maajabu
Christina Gauluhanga na Stella Aron, jijini
JIJI la Dar es Salaam leo lilikumbwa na shamshara na nderemo katika baadhi ya maeneo kutokana na wagombea wa vyama vitatu kurejesha fomu za kuwania nafasi ya rais.
Wagombea hao walikuwa wakirejesha fomu kwa nyakati tofauti katika ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
|
|
Wananchi waaswa kutotumia maziwa haya |
|
Thursday, 19 August 2010 11:12 |
|
Na Christina Gauluhanga, jijini
WANANCHI wametakiwa kuwa makini na utumiaji wa maziwa ya watoto wadogo ambapo yameibuka feki na yanaweza kuhatarisha afya za watoto.
Katika taarifa iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari imeonesha kuwa, uhalisi wa maziwa ya Nestle umeoneshwa kwenye kopo la maziwa hayo na NAN 2, LACTOGEN 1 Na LACTOGEN 2 yanatengenezwa na Nestle ya Ufaransa, NAN 1 inatengenezwa na Nestle ya Netherlands
|
|
|
|
|
<< Start < Prev 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 Next > End >>
|
|
Page 12 of 47 |