Home
Dar Leo
TAA
Tuesday, 17 August 2010 12:26

Fundi umeme akitengeneza moja taa za barabarani mtaa wa Msimbazi  jana taa hizo ziliwekwa na baadhi ya makampuni binafsi nyingi hazifanyi kazi kutokana na kukosa matengenezo. (Picha na Charles Lucas)

 
Aua mke wake kwa wivu wa mapenzi
Tuesday, 17 August 2010 12:20

Na Mwandishi Wetu, Mara

POLISI mkoani Mara linamshikili Shelistika Bisheke (40) kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumkata na panga kichwani na kusababisha ubongo kutoka nje.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana katika Wilaya ya Musoma mkoani Mara.

Imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alimfuata mkewe, Kemista Shelistika (30), ambaye walikuwa wametengana kwa kipindi cha miaka miwili.

 
Jambazi lajinyonga
Tuesday, 17 August 2010 12:18

*Lamuiga Chifu Adam Sappi Mkwawa
*Risasi 30 na bastola zakutwa pembeni yake

Na Waandishi Wetu, Mbeya

MWANAMUME mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi sugu, Maneno Mwamsojo 'Sojo' (38), ametoa kali baada ya kujiua kwa kujinyonga kwa kitanzi cha kamba ya katani kwenye  mti porini ili asikamatwe na polisi akiwa hai.

Kifo cha Sojo, ambaye inadaiwa alikuwa ni ‘kipusa adimu’ kilichokuwa kikisakwa na polisi kwa muda mrefu ambapo kwa mara ya mwisho alipigwa risasi ya goti na kutoweka, kimefananishwa na cha mtemi wa Wahehe, Chifu Adam Sapi Mkwawa, ambaye aliamua kujinyonga ili asikamatwe na maadui zake Wajerumani wakati wa vita.

 
Polisi ‘feki’ wavamia hoteli Dar
Tuesday, 17 August 2010 12:19

Na Waandishi Wetu, jijini

WATU wawili waliojifanya ni askari Polisi wamevamia katika hoteli ya Nyanyamo iliyopo Ilala na kuwapora wateja vitu mbalimbali pamoja na fedha ambayo thamani yake bado haijafahamika.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, tukio hilo limetokea juzi saa 5 usiku katika mtaa wa Agrey kwenye hoteli hiyo.

 
Mdee awaasa wakazi Dar
Tuesday, 17 August 2010 12:17

Na Mwandishi wetu, jijini

MGOMBEA ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee, amewataka wakazi wa Dar es Salaam kukumbuka historia ya ari ya siasa za mageuzi waliyowahi kuwa nayo ili waitumie kuleta mabadiliko ya uongozi nchini.

Amesema wakazi wa Dar es Salaam wanapaswa kuwa watu wa mfano wa kuigwa katika kutetea mabadiliko nchini.

 
<< Start < Prev 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 Next > End >>

Page 13 of 47

Swali la Leo

Website is used for?
 

Walio Kwenye Mtandao

We have 18 guests online
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday462
mod_vvisit_counterYesterday768
mod_vvisit_counterThis week1636
mod_vvisit_counterLast week5276
mod_vvisit_counterThis month4673
mod_vvisit_counterLast month22527
mod_vvisit_counterAll days53293

We have: 16 guests, 2 bots online
Your IP: 38.107.191.107
 , 
Today: Sep 07, 2010