|
Shule iliyokumbwa na mashetani |
|
Tuesday, 31 August 2010 11:20 |
|
Na Waandishi Wetu, Tabata
BAADA ya zaidi ya wanafunzi 26 wa Shule ya Msingi Tumaini kuanguka jana na maruhani leo shule hiyo ilionekana kupwaya baada ya wanafunzi kutofika shuleni wakihofia kukumbwa na masaibu hayo.
Gazeti hili leo asubuhi lilishuhudia shule hiyo ikiwa na idadi ndogo ya walimu na wanafunzi, hali ambayo ilizidi kuifanya shule hiyo kuzizima kutokana na ukimya uliokuwapo.
Imebadinika kuwa baadhi ya wazazi wamelazimika kuwakataza watoto wao kwenda shule kwa kuhofia kukumbwa na balaa hilo.
|
|
|
Wanasiasa walaumu vyombo vya habari |
|
Tuesday, 31 August 2010 11:18 |
|
*Wadai wanaibeba CCM, CUF na CHADEMA
Na Dunstan Bahai, jijini
WAKATI zimetimia siku 11 leo tangu kuanza kwa kampeni, baadhi ya vyama vya siasa vimelalamikia vyombo vya habari kuwa vinapendelea kutoa taarifa za vyama vyenye fedha.
Hayo yamesemwa na mgombea urais kwa tiketi ya chama cha APPT, Peter Mziray, na kuongeza kuwa siku ambayo Chama cha Wananchi (CUF) kilipokuwa kikizindua kampeni zake, chama chake nacho kilikuwa kinafanya uzinduzi Mbagala, lakini hakukuwa na vyombo vya habari na badala yake vyombo vingi vilikimbilia CUF.
“Chama changu hakina bajeti ya waandishi wa habari. Vyama vingine vina bajeti, siwezi kuahirisha kampeni zangu eti tu kwa vile sina bajeti ya vyombo vya habari,” amelalamika mgombea huyo.
|
|
Tuesday, 31 August 2010 11:12 |
|
Na Shufaa Lyimo, jijini
MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba na Taifa Stars, Uhuru Selemani, amesema baada ya kutemwa timu ya Taifa 'Taifa Stars', sasa mawazo yake ameyapeleka katika mechi yao dhidi ya Azam FC Septemba 11, mwaka huu.
Uhuru aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam mara baada ya kutemwa na Kocha Mkuu wa Stars Mdernmark Jan Poulsen na kwamba, ni jambo la kawaida kwa kocha kutema baadhi ya wachezaji kulingana na mahitaji yake.
|
|
|
Joseph apania makubwa Algeria |
|
Tuesday, 31 August 2010 11:14 |
|
Na Mohamed Akida, Sinza
KIUNGO wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', na klabu ya Kongsvigers ya Norway, Henry Joseph, amesema kuwa, wana uhakika wa kufanya vizuri katika mechi ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Algeria.
Stars inaondoka leo kwenye nchini Algeria inatarajiwa kushuka dimbani Septemba 3, mwaka huu kucheza na Algeria ambao walishiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Akizungumza na gazeti hili jana, Joseph alisema kutokana na uzoefu alioupata kupitia soka la Ulaya, wana uhakika wa kuipeperusha vizuri bendera ya Taifa na kuibuka na ushindi.
|
|
Tuesday, 31 August 2010 11:10 |
|
MADRID, Hispania MSHAMBULIAJI wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki tatu kutokana na kuumia kifundo cha mguu 'ankle', klabu huyo inayocheza Ligi Kuu Hispania 'La Liga' imethibitisha.
Ronaldo, 25, aliumia wakati wa mechi ya La Liga iliycohezwa Jumapili dhidi ya Real Mallorca na kuchukulia vipimo jana ambapo vilionesha kuwa ameumia.
Wakikadiria siku za kupata nafuu, kati ya wiki tatu, Ronaldo sasa ataikosa mechi ya timu ya taifa ya Ureno dhidi ya Cyprus na Norway za kusaka tiketi ya kucheza fainali za Mataifa ya Ulaya 'Euro 2012.
Pia, mshambuliaji huyo atakuwa nje katika mechi ya Real Madrid dhidi ya Osasuna na Klabu Bingwa dhidi ya Ajax.
Ingawa kocha Jose Mourinho atamkosa Ronaldo, atawatumia Karim Benzema na mshambuliaji aliyesajiliwa majira ya joto Mesut Ozil.
|
|
|
|
|
<< Start < Prev 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 Next > End >>
|
|
Page 2 of 47 |