HUU HAPA UKWELI WA RAIS SAMIA KUJENGEWA SHULEWananchi wa kata ya Majengo wamejikusanya fedha na kuanza ujenzi wa shule mpya ya msingi ambayo wanampango wa kuita shule ya mama Samia Hassan Suluhu ambaye ni Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa kutambua mchango wake wa kuleta maendeleo nchini ambayo inawagusa mpaka wananchi wa jimbo la Tunduma.

Hayo ameyasema Diwani wa kata hiyo Frank Mponzi wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa TAMISEMI na mbunge wa jimbo la Tunduma David Silinde na kusema wao kama wananchi wameamua kujenga shule mpya ya msingi kutokana watoto wengi hutembea umbali mrefu kwenda shule hivyo shule hiyo itawarahisishia watoto hao kusoma.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauli ya Mji wa Tunduma Regina Bieda amesema kwasasa wamewaingizia milioni 10 kuanza ujenzi huo baada ya Wananchi kufyatua matofali elfu sabini tano na kua na eneo hivyo ujenzi huo utaanza mda wowote na ifikapo january shule hiyo itaanza kutoa huduma.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Tunduma na Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde amesema ujenzi wa shule hiyo ya msingi ya mama Samia wao kama serikali watajibu hilo kwa kutafuta fedha ili shule hiyo ikamilike maana hata Rais akisikia atafurahi kuona wananchi wameipa shule jina lake,kwahiyo waanzishe ujenzi serikali itasaidia na Tunduma iwe ya mfano katika sekta ya elimu.

Akikagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita ambayo ipo katika kata ya Maporomoko ambayo itagharimu kiasi cha bilioni moja amesema amelidhishwa na kasi ya ujenzi huo na kuagiza ikmailike kwa wakati iruhusu wanafunzi kuanza kutumia na itakua na uwezo wa wanafunzi kuweza kulala shuleni hapo na nyumba za walimu na kila kitu kinachoitajika shuleni na itakua ya kisasa huku akitarajia shule mpya nyingine jimboni ambayo itakua ya wasichana tupu .

No comments

Powered by Blogger.