MWALIMU ASIMAMISHWA KAZI KWA KUMTUKANA RAIS SAMIANA MWANDISHI WETU

 Mwalimu Shela Mwangoka wa shule ya sekondari ya momba katika wilaya ya momba mkoa wa Songwe amesimamishwa kazi na Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde kwa kudaiwa kumtusi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika kadamnasi ya watu kwa dhihaka kwa lugha zisizofaa kwa Rais.


Hayo yamebainika baada ya mkutano wa shina kati ya wananchi wa kijiji cha washo kata ya myunga wilaya ya Momba Emily Skanyika na Jacob Miyala ambao walitoa kero yao kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa CCM Shaka Hamdu Shaka kua mwalimu huyo amekua akitoa lugha za matusi mara kwa mara hali ambayo inawachafua wananchi hao kuona Rais wao anatukanwa na kuwa aliwamabia "Rais wenu Mpumbavu ameniongezea madaraja ili nimuunge mkono".


Kwa upande wake Naibu waziri wa TAMISEMI David Silinde amesema amefanya uchunguzi mdogo baada ya kusikia malalamiko hayo kujiridhisha na kugundua kua ni tabia ya Mwalimu huyo kufanya hivyo na mala ya mwisho ni hata wiki moja aijapita akiwa sokoni alipoona Rais Samia kaongeza madaraja na mishahara kwa watumishi wa umma akasema ni hongo ili amuunge mkono akasema awezi muunga mkono sababu ni mwanamke.


Hatuko tayari kufanya kazi na watu ambao hawaheshimu mamlaka,nimemuagiza afisa elimu wa wilaya ya Momba huyu mwalimu anasimamishwa kazi kuanzia leo na baada ya hapo hatua nyingine za kidhaamu zitafatwa ikiwemo jambo lake kupelekwa katika tume utumishi ya walimu" Naibu waziri Silinde.


Kwa upande wake katibu wa itikadi na uenezi Taifa CCM Shaka Hamdu Shaka amesema haiwezikani mtu mmoja au kikundi cha watu kumdhalilisha Rais na ametaka watumishi wa umma wenye tabia kaa hizo ambao hawana maadili na nidhamu wabadilike vinginevyo watachukuliwa hatu kali za kinidhamu juu yao.

1 comment:

  1. Inter huyo mwalimu anaonekana hakuwa na malezi bora, hivyo asituharibie watoto wetu, pia uwezo wake wakupambanua mambo ni mdogo, huyu ni matunda ya upe

    ReplyDelete

Powered by Blogger.