NAIBU WAZIRI MABULA AITAKA MANISPAA MPANDA KUANDAA MPANGO KAZI KUTEKELEZA MPANGO KABAMBE

Na Munir Shemweta, KATAVI

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Dkt Angeline Mabula ametoa wito kwa halmashauri ya na Wadau wa maendeleo katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kuandaa mkakati na mpango kazi wa utekelezaji mpango kabambe.

Dkt Mabula alitoa wito huo tarehe 20 Julai 2021 wakati wa uzinduzi wa Mpango Kabambe wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri mkoani humo.

Aidha, aliitaka halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kutafuta wabia na wawekezaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta mbalimbali zilizoainishwa kwenye Mpango Kabambe.

‘’Nitoe wito kwa taasisi zinazotoa huduma mbalimbali katika Manispaa ya Mpanda kuutumia Mpango Kabambe ulioandaliwa katika utekelezaji shughuli zao na miradi ya maendeleo’’ alisema Dkt Mabula

Aliitaka halmashauri ya Manispaa ya Mpanda katika mkoa wa Katavi kuendelea kuratibu utekelezaji Mpango Kabambe aliouzindua kwa kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ya Manispaa.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, Kifungu cha 4 (3) cha sheria ya mipango miji ya mwaka 2007 kinazitaka Mamlaka za upangaji yaani Mamlaka za miji midogo, Manispaa na Majiji kuandaa ripoti za utekelezaji wa Mipango Kabambe na kuiwasilisha kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi kila mwaka na kubainisha kuwa ripoti hiyo haiwezi kutayarishwa bila ya kuwa na mipango na mikakati mahsusi ya utekelezaji.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu kwa upande wake alisema, mkakati wa utekelezaji mpango kabambe wa Manispaa ya Mpanda 2018-2038 unatekelezwa kwa awamu tatu na kuainisha vyanzo vya mapato kwa ajili ya utekelezaji wake ni kutoka mapato ya ndani ya halmashauri.

Nzyungu alitaja vyanzo vingine kuwa ni kutoka serikali kuu, ubia na sekta binafsi, mifuko ya barabara pamoja na wafadhili mbalimbali. Wakati huo huo, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezindua na kuukabidhi ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi. Ukumbi huo umejengwa na shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa gharama ya shilingi milioni 367.Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikabidhi Mpango Kabambe wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi kwa Mkurugenzi wa Manispaa Michael Nzyungu (kushoto) na Meya wa Manispaa hiyo Haidari Subi wakati wa uzinduzi uliofanyika wilayani Mpanda mkoani Katavi jana.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akionesha Mpango Kabambe wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi mara baada ya kuuzindua jana.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikata utepe kuzindua ukumbi wa halmashauri ya Manispaa ya Mpanda jana mkoani Katavi uliojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
……………………………………………………
Na Mwandishi wetu
Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema dhamira ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona zvyombo vya Habari vinaendelea kufanya kazi kwa uhuru lakini vizingatie Sheria zilizopo nchini.
Ameyasema hayo leo Julai 20, 2021 wakati akizungumza mubashara kwenye kipindi cha Clouds 360 kilichorushwa Kituo cha Televisheni cha Clouds.
“Matarajio yangu ni kwamba vyombo vya habari vitazingatia Sheria hii na nimeshakutana na wadau mbalimbali wa habari juu ya utekelezaji wa Sheria hii na Mhe. Rais ameshatoa maelekezo kuwa wale waliomaliza adhabu zao wapewe leseni waendelee na kazi zao”, alisema Msigwa na kuongeza kuwa tayari Idara ya Habari inakamilisha taratibu za Kidheria ili Vyombo hivyo vianze tena kufanya kazi.
Amesema wakati wa kipindi chake kama Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali vyombo vya habari vifanye kazi kwa bidii na vijivunie kuelezea maendeleo ya nchi yao.
“Ni lazima sisi waandishi wa habari pamoja na majukumu yetu na taratibu zetu za kitaaluma tuna wajibu wa kimsingi wa sisi kama watanzania kuitanguliza nchi yetu mbele”, amesisitiza Msigwa.
Kwa upande mwingine amesema kuwa kuna mchakato unaendelea ndani ya Serikali kuhakikisha eneo la kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya masuala ya habari na mawasiliano linarahisishwa ili vijana wengi waweze kujiajiri na kufanya mambo yao huko.

No comments

Powered by Blogger.